10. "EFATHA" - FUNGUKA (Mk 7:31 - 37)



TAARIFA MUHIMU: Mtu katika kifungu hiki hakika alikuwa kiziwi tangu mwanzo wa utoto wake. Kwa sababu hiyo, alishindwa kuwasiliana na watu wengine. (Nyakati hizo bado hakukuwa na lugha ya bubu inayotumika sana.) Isaya alikuwa ametabiri miaka 700 iliyotangulia kuwa Masihi angewafanya viziwi kusikia na mabubu kusema (37, linganisha na Isa 35:5).

1. Zifikirie aina za sauti unazozisikia mchana kutwa. Unafikiri ni nini kingekuwa shida zaidi kwako kama hukuwa na uwezo wa kusikia chochote?

2. Fikiria maisha ya utotoni ya mtu huyu jinsi yalivyokuwa. (Ni uwezo gani uliokuwepo ambao wazazi wake waliutumia kumfunza mtoto wao ili kumkinga dhidi ya hatari, kumfanya aifanye kazi n.k.? Ni uhusiano wa aina gani aliokuwa nao na wenzi wake? Unafikiri kujistahi kwake kulikuwaje?)

3. Yalinganishe maisha ya kiziwi huyu na maisha ya wenzi wake alipokuwa mtu mzima.
  • Labda mtu huyu pia alikuwa ameitembelea sinagogi au hekalu mara chache. Unafikiri aliyaelewa mangapi kuhusu Mungu asiyeonekana?

    4. Je watu waliomleta kwa Yesu walikuwa na nia gani? Ufikirie uwezekano mbalimbali (31 - 32).
  • Iwapo ni wewe uliyetaka kumleta kiziwi huyu kwa Yesu, ungemwelezeaje mahali mlikuwa mnampeleka na kwa nini?

    5. Kwa nini Yesu hakumponya kiziwi huyu kulingana na jinsi marafiki zake walivyomwuliza 32 -34)?
  • Kwa nini mtu huyu hakukataa na badala yake alimfuata Rabi ambaye hakumjua (33)?
  • Kwa nini Yesu alitaka kumpeleka kiziwi huyu kando, mbali kutoka kwa umati (33)?

    6. Unafikiri kiziwi huyu aliyaelewa mangapi miongoni mwa ishara nne za Yesu za lugha ya bubu katika aya ya 33 - 34? (Ni nini Yesu alitaka kukiwasilisha kwa kiziwi huyu alipoyagusa masikio yake - ulimi wake - alipotazama mbinguni - aliposhusha pumzi kwa nguvu kabla ya kumponya?)

  • Unafikiri ni kwa nini Marko aliliandika neno la kuponya la Yesu kwa Kiaramaiki cha asili katika injili yake (34)?

    7. Ni mambo gani yanayokuzuia kuyasikia yale watu wengine wanajaribu kukwambia hata kama uwezo wako wa kusikia ni mzuri sana?

  • Yesu anasimama mbele yako sasa na anakwambia: "Efatha!" - "Funguka!" Anamaanisha nini - fikiria kuhusu mawasiliano yako na watu wengine. (Unaweza kujibu kimoyomoyo.)

    8. Kwa kawaida inamchukua mtoto miaka mitatu kujifunza maneno muhimu zaidi ya lugha. Inawezekanaje kuwa kiziwi huyu alizipata habari hizo mara moja tu (35)?

    9. Kila muujiza wa Yesu unatufundisha jambo fulani juu ya mbinguni. Tunajifunza nini kuhusu mbinguni katika tukio hili?

    10. Kwa nini watu waliendelea kuongea kuhusu muujiza huu ingawa Yesu alikuwa amewaagiza wasiseme chochote (36)?
  • Yesu angependelea watu wawaambie wenzao nini kumhusu?
  • Unafikiriaje: kuna faida kwa kanisa la Kikristo la nyakati hizi zetu kuitangaza miujiza katika vyombo vya habari?

    11. HABARI NJEMA: Mawasiliano ya kina baina ya Yesu na Mungu yalikatishwa Yesu aliponing’inia msalabani na Mungu aliyafunga masikio yake kwa kilio chake. Mungu huwasikia tu wenye haki na wakati huo Yesu alikuwa mwenye dhambi kuliko wengine wote sio kwa sababu ya dhambi zake mwenyewe bali dhambi zetu. Kunyamaza kwa Mungu kulikuwa gharama aliyoilipa Yesu kwa kuyaanzisha tena mawasiliano kati yetu wenye dhambi na Mungu wetu mwenye haki.

    ***

    ? 2009 Glad Tidings Bible Studies in Swahili - www.gladtidings-bs.com