1. YESU ANAKUTANA NA MTUMISHI WA SERIKALI MDANGANYIFU (Mt 9:9 -14)
TAARIFA MUHIMU: Kula pamoja kulikuwa ishara ya urafiki miongoni mwa Wayahudi wakati wa Yesu. Watu wa dini waliwadharau watoza ushuru kwa sababu walikusanya ushuru kwa sababu ya wanajeshi wakaaji wa Warumi. (MONGOLIA). Hawa ni sawa na Wamongolia wanaoishi upande wa Uchina ilhali Mongolia ilikuwa chini ya utawala wao. Isitoshe, watosha ushuru waliwatosha watu ushuru kupita kiasi na waliyachukua masalio. Mathayo alikuwa amefundishwa kuhusu Amri Kumi katika Biblia. Kwa mfano: Usiibe! Mfarisayo alikuwa kiongozi wa kidini.
1. Je, mtu anaweza kuwa mwenye furaha kama hana pesa za kumwezesha kuishi kwa starehe?
Yafikirie maisha ya Mathayo, mtosha ushuru. Ni mambo gani ambayo hayakuwa mazuri katika maisha yake licha ya mshahara wake mkubwa?
Mathayo aliweza kufikiria nini kuhusu Mungu na Amri zake alipokuwa anaifanya kazi yake kama mtosha ushuru?
Kwa nini ni kawaida kwa watu kuzichukua pesa na vitu vinginevyo visivyokuwa vyao wakati huu wetu?
2. Mathayo alitarajia Yesu aseme nini alipoingia ofisini mwake?
Kwa nini Yesu alimwuliza Mathayo: "Ungependa kuwa mfuasi wangu?"
Mathayo alifikiria nini wakati kiongozi mashuhuri wa kidini alipomwuliza ajiunge na wafuasi wake?
Kwa nini Yesu alitaka kuwa na mtosha ushuru mmoja miongoni mwa wanafunzi wake ingawa alijua kuwa angekosolewa kwa kufanya hivyo?
3. Wenzi wa Mathayo walifikiria nini alipoiacha kazi yake ghafla bila hata kuviondoa vitu vyake kutoka katika dawati lake?
Nini kilichomtia moyo Mathayo kuiacha kazi yake nzuri na mapato ya mara kwa mara?
4. Mathayo alipokea nini badala ya vitu alivyovipoteza alipomfuata Yesu?
Maisha ya mke na watoto wake yalibadilikaje wakati aliyewapatia riziki yao ya kila siku alikuwa mfuasi wa Yesu?
Kwa nini Mathayo alitaka kuipanga karamu ya chakula ambapo aliwaalika Yesu na wenzi wake wa zamani (10)?
5. Ni akina nani katika jamii yetu ambao watu wa heshima hawataki kuchangamana nao (11)?
Kwa nini Yesu alitaka kuchangamana na watu wa kila aina?
6. Kwa nini Mafarisayo hawakumkosoa Yesu moja kwa moja bila kuogopa na badala yake waliwakosoa wanafunzi wake (11)?
7. Yesu alimaanisha nini katika haya ya 12 - 13?
Unastahili kuwa wapi kati ya vikundi hivi viwili: cha haki au cha wenye dhambi? (Unaweza kujibu kimoyomoyo.)
8. Baadaye Mathayo hata aliuandika wasifu wa Yesu: Injili ya Mathayo. Unafikiri alisikitika kwa kuviacha vitu vyote na kumfuata Yesu? toa sababu zako.
9. MASWALI YA HABARI NJEMA: Sasa Yesu anakuambia mambo haya mawili: "Nifuate!" na "Sikuja kuwaita watu wema bali wenye dhambi." Unamjibu nini?
(Kwa kila mshirika kujibu): Ni jambo gani muhimu zaidi ulilojifunza kutokana na haya Mafundisho ya Biblia?
***
? 2009 Glad Tidings Bible Studies in Swahili - www.gladtidings-bs.com