17. YESU ANAKUTANA NA MWANAFUNZI MWENYE MASHAKA (Yn 20:19 - 29)
TAARIFA MUHIMU: Thomaso alikuwa mmoja wa wanafunzi kumi na wawili wa Yesu. Labda alikuwa na ndugu pacha kwa sababu jina lake linamaanisha "pacha".
1. Mwanadamu anaweza kuwa na maisha mema katika ulimwengu huu bila kuamini kuwa mwili wake utafufuka kutoka kaburini siku ya mwisho?
Ni tabia nzuri zipi zipatikanazo katika nafsi ya mtu kama Thomaso? Tabia mbaya ni zipi?
Unafikiri ni kwa nini Yesu alimchagua mtu kama huyu kuwa mmoja wa wanafunzi wake?
2. Wanafunzi walifikiria nini kuhusu Yesu asubuhi na mchana wa Jumapili ya Pasaka?
Kwa nini wanafunzi hawakuamini katika ufufuo wa Yesu?
Yafikirie maelezo mbalimbali kuhusu pahali ambapo Thomaso angekuwa ameenda Jumapili jioni alipokuwa hayupo pamoja na wanafunzi wengine kumi (24).
Kwa nini Yesu aliyefufuka aliwaamkua wanafunzi wake kwa kusema, "Amani iwe nanyi" (21, 26)
3. Ufufuo ulikuwa umetabiriwa na manabii wa Agano la Kale na Yesu mwenyewe. Sasa marafiki wa dhati wa Thomaso walimhakikishia kuwa walikuwa wamemwona Yesu kwa macho yao yenyewe. Kwa nini Thomaso hakuamini katika ufufuo wa Yesu hata baada ya kuusikia ushuhuda huu wote (25a)?
Kama ungekuwa katika hali ya Thomaso, unafikiri ungeuamini ufufuo? Toa sababu zako.
4. Unafikiri Thomaso alijihisi vipi juma lililofuata miongoni mwa marafiki zake walioshangilia?
Ni nini kilichomfanya Thomaso kukaa na marafiki zake badala ya kujiendea zake juma hilo hiyo?
Je, ni nini kingetokea kwa Thomaso iwapo angekiacha kikundi cha wanafunzi wakati huu?
Ni nini kitakachotokea kwetu iwapo tutauacha ushirika wa Kikristo tunapokuwa na mashaka kuhusu mafundisho ya dini ya kimsingi ya Kikristo?
6. Kwa nini Thomaso alitaka kumgusa Yesu kabla ya kuamini katika ufufuo wake (25b)?
7.
Unafikiri Thomaso alihisi vipi alipoyasikia maneno yake mwenyewe kutoka kinywani mwa Yesu (25 - 27)?
6. Ni maelezo yapi ya kinaganaga yanayotuonyesha kuwa Yesu alikuwa si ziwi wala pepo (27)?
Unafikiri kwa kweli Thomaso aliviweka vidole vyake katika makovu ya mikononi na ubavuni mwa Yesu?
7. Thomaso alikuwa mtu wa kwanza katika Agano Jipya kumwita Yesu Mungu sio tu Mwana wa Mungu (28). Kwa nini Wakristo wote ulimwenguni wanaamini kuwa Yesu ni Mungu?
8. Yesu anamtaja nani katika aya ya 29?
Kwa nini ni muhimu kuuamini msaada wa Mungu kabla ya kuupokea?
9. Kulingana na kifungu hiki, Yesu anamtendeaje mtu anayependa kumwamini lakini hawezi?
Ungemjibu nini mtu aliyesema kwako: "Ninamwamini Yesu lakini siamini katika ufufuo wake wa mwili"?
Kwa nini imani yote ya Kikristo inaporomoka iwapo mwili wa Yesu haukufufuka kutoka kaburini?
10. MASWALI YA HABARI NJEMA: Thomaso alisema kwa Yesu: "Bwana wangu na Mungu wangu!" Unaweza kulifanya ungamo sawa kwa Yesu leo? (Unaweza kujibu kimoyomoyo.)
(Kwa kila mwana kikundi kujibu): Ni jambo gani muhimu zaidi ulilojifunza kutokana na haya Mafundisho ya Biblia?
***
Version for printing
Downloads
Contact us
Webmaster