14. KICHEKO KIITWACHO HUKUMU YA YESU (Mk 15:1 - 15)
TAARIFA MUHIMU: Kuna maswali mengi sana katika somo hili ambayo huwezi kuyauliza yote katika kipindi cha saa moja. Wachague wahusika wawili au watatu kutoka kikundi kwa majadiliano yenu. Au badala yake kigawe kikundi chako cha Mafundisho ya Biblia katika vikundi vya washirika 2 au 3. Kila kikundi kijadiliane kuhusu wahusika wawili au watatu na kisha kishiriki matokeo yake na vingine.
1. PONTIO PILATO
Kama gavana wa Yuda mwaka wa 26 - 36 BK, aliwawakilisha wanajeshi watawala wa Himaya ya Warumi na aliwajibika kwa Mfame Tiberia mwenyewe. Pilato hakutaka mfalme ausikie uvumi wowote kuhusu maasi ya Wayahudi. Ilikuwa haki yake kuitangaza adhabu ya kifo au kuinyima.
Aya ya 1 - 15
Ni mawazo yapi unayoyapata kuhusu tabia za Pilato na maadili yake?
Unafikiria nini kuhusu jaji anayeyauliza mawsali kama yale yanayoulizwa katika aya ya 12 na ya 14 wakati wa hukumu?
Kwa nini Pilato hakuutumia uwezo wake na badala yake aliwaruhusu wengine wamtolee uamuzi?
Unafikiri Pilato alifikiria nini kuhusu Yesu? (Kwa nini alimwita Yesu "Mfalme wa Wayahudi" mara mbili? (linganisha aya ya 9 na ya 12.)
Walinganishe hawa watu wawili: Gavana wa Kirumi na Mfalme wa Wayahudi. Kuna tofauti za kuvutia zipi kati yao katika hali hii?
Ni nani aliyeisuluhisha kesi hii rasmi mwishoni?
Unafikiri Pilato alihisije alipomtoa Yesu achapwe mijeledi na asulubiwe (15)?
Unafikiri Pilato alijaribuje kuituliza dhamiri yake maishani mwake?
Kama ungekuwa katika hali ya Pilato asubuhi ile ungeiamuaje kesi hii?
2. BARABA
Mwuaji na kiongozi wa uasi kisiasa, jina lake linamaanisha mwana wa baba.
Aya ya 6 - 15
Yafikirie maisha ya utoto, ya ujana na ya utu uzima ya mtu huyu. Ni nini labda kilichomfanya Baraba kuwa mwanamapinduzi na mwuaji?
Iwapo hali zako zingekuwa tofauti, unafikiri mwenyewe ungekuwa mwuaji? Kwa nini? Kwa nini hungekuwa?
Unafikiri ni mawazo gani yalizokuwa zinaendelea akilini mwa Baraba wakati siku ya kuuawa kwake ilipokuwa inakaribia? (Unafikiri alijuta kwa lolote?)
Unafikiri Baraba alienda kumwona mtu aliyesulubiwa msalabani badala yake?
Ni kwa njia gani sote tunafananishwa na Baraba katika mahusiano yetu na Yesu?
3. MAKUHANI WAKUU
Kwa kawaida kulikuwa na kuhani mkuu mmoja kila wakati lakini katika hali hii, kulikuwa na wawili: Kayafa, kuhani mkuu halisi katika mwaka wa 18 - 36 BK na baba mkwe, Anasi aliyeyashikilia mamlaka awali. Anasi bado aliutumia ushawishi wake kupitia kwa mkwe wake.
Aya ya 1 - 15
Unafikiri ni nini kuhani mkuu alikichukulia kuwa wito mkuu maishani?
Kwa nini Kayafa na Anasi walimwonea Yesu wivu?
Kwa nini makuhani wakuu hawakuitambua nia yao?
Ni uvunjaji sheria upi uliokuwa mbaya zaidi: hukumu ya kifo isiyo haki iliyotekelezwa na makuhani wakuu au mauaji aliyokuwa ameyatekeleza Baraba wakati wa uasi?
Ni nini kinachoweza kumfanya mtu wa dini sana kuwa chombo cha ibilisi?
Unafikiri unawafanana makuhani wakuu kwa njia yoyote? Iwapo unawafanana, ni kwa njia gani?
4. UMATI
Walipiga kelele, "Hosana" kwa Yesu Jumapili iliyokuwa imetangulia. Sasa wanapaaza sauti: "Msulubishe!" Lazima kulikuwa na wengine miongoni mwa umati huu waliokuwa wamesaidiwa na Yesu.
Aya ya 8 - 15
Kwa nini umati ulimtaka muuaji hatari aachiliwe huru?
Watu waliwezaje kukubali kumshambulia mfadhili wao? (Kwa nini kulikosekana hata sauti ya mtu moja iliyomtetea Yesu dhidi ya hila za haki katika hali hii?)
Je, ungefanya nini kama ungekuwa miongoni mwa umati asubuhi hiyo?
Unafikiri tendo kama hili lingetokea katika nchi yako wakati huu? Toe sababu zako?
Aya hii kinatufundisha nini kuhusu uzuri na ubaya wa demokrasia?
5. YESU
Anaisema sentensi moja tu wakati wa hukumu nzima (2). Kwa upande mwingine, ananyamaza.
Aya ya 1 - 15
Kufikia wakati huu, Yesu alikuwa amelikataa jina lolote isipokuwa "Mwana wa Mtu". Kwa nini sasa anakubali hadharani kuwa yeye ni mfalme wa Wayahudi (2)?
Kwa nini Yesu hajitetei mwenyewe?
Mlinganishe Yesu na watu wengine katika kifungu hiki. Je, anatofautianaje nao? (Ni nini kinachomfanya Yesu astaajabiwe hasa unapoizingatia hali yake?)
Unafikiri Yesu alihisi nini dhidi ya wale watu wote waliomzunguka na waliokuwa na hamu ya kuimwaga damu?
Ni nani aliyeamua kesi ya Yesu wakati wa hukumu yake: Pilato, Mungu au shetani?
***
Version for printing
Downloads
Contact us
Webmaster