13. UPENDO HAUTAWEZA KUSHINDWA (Mk 14:1 - 9)
TAARIFA MUHIMU: Kiongozi aelezee kwa kifupi mistari ifwatayo inatufunza nini kuhusu Maria wa Bethania. Lk 10:38 - 42, Yn 11 na Yn 12:1 - 11. (Maria huyu asichanganywe na mamake Yesu au mwanamke anayezungumziwa katika (Lk 7:36 - 50). Wazazi wa Martha, Maria na Lazaro dhahiri walikuwa wamekufa. Waliwaachia mabinti zao pesa za kutumia labda wakati wangeolewa au za kuwasaidia wakati za uzeeni. Juma la mwisho ya maisha ya Yesu ulimwenguni ilikuwa inaanza tu.
1. Ni zawadi gani ungependa kumpa rafiki yako iwapo ungejua kuwa angekufa?
Yesu anayataja maziko yake hapa (1 - 2, 8)? Unafikiri Maria, tofauti na wanafunzi, alitambua kuwa angekufa karibuni? Toe sababu zako.
2. Ili kuyanunua marashi ya nardo, ungekilipa kiasi cha pesa ambacho kingelingana na wastani ya mshahara ambao mfanyakazi angeupokea kwa mwaka mzima (3). Hii ndiyo sababu tone moja moja tu la mafuta haya lilitumika. Chupa hii ingeuzwa kiasi gani cha pesa ukilinganisha na sarafu zetu leo?
Kwa kawaida inachukua muda gani kuziweka pesa zinazoweza kulingana na mshahara wa mwaka mmoja?
Maria alipoyanunua marashi haya ghali, alikuwa akifikiria nini kuhusu mahari yake au malipo yake ya uzeeni?
3. Kwa nini Maria aliyamwaga mafuta yote katika kichwa cha Yesu badala ya matone machache tu (3 - 4)?
Maneno "Masiya" na "Kristo" yana maana ya "aliyepakwa mafuta". Wafalme wa Wayahudi kawaida walikuwa wanapakwa mafuta mwanzoni mwa kazi zao. Kwa nini Yesu hakupakwa mafuta hadi muda mfupi tu kabla ya maziko yake?
4. Maria alikuwa ameitumia akiba yake yote kwa chupa ya marashi. Ni sehemu gani ya kumkosoa iliyomuudhi zaidi (4 - 5)?
Mshahara wa mwaka mmoja ungetumiwaje kuwafaidi maskini wa mji (5)? Ufikirie uwezekano tofauti tofauti.
5. Yesu alimtetea Maria kwa njia mbalimbali zipi (6 - 9)?
Unafikiri Yesu angekwambia alivyomwambia Maria: "Yeye amefanya alivyoweza" (8)?
Ungemfanyia Yesu nini kutoka sasa na kuendelea?
6. Tendo la Maria na tendo la Yesu yanafananaje (kifo chake msalabani, k.m. “injili" katika aya ya 9)?
Unafikiri ni "hasara" gani iliyo kubwa: kwamba Maria aliyamwaga marashi yake ghali kwa ajili ya Yesu au kwamba Yesu aliimwaga damu yake kwa ajili ya Maria?
7. Ni jambo gani lililo la kipekee sana litakalokumbukwa milele katika tabia za Maria (9)?
Ni kumbukumbu gani ungependa kuiacha utakapokufa?
8. Unafikiri Maria alihisi vipi baadaye kuhusu pesa "alizozipoteza" kwa ajili ya Yesu siku hiyo?
Maria alijifunzaje kumpenda Yesu sana?
Tunawezaje kujifunza kumpenda Yesu jinsi Maria alivyompenda?
9. HABARI NJEMA: Maria alikuwa amejifunza kumpenda Yesu kwa kumsikiliza. Hiyo ndiyo sababu pia aliweza kumhudumia wakati uliofaa. Kwanza, Maria alikuwa ameamini kusamehewa kwa dhambi zake na imani hii yake ndiyo iliyomfanya akitoe kila alichokuwa nacho kwa Bwana. Ilikuwa ni kwa sababu yake Yesu alitembea akiwa na harufu ya marashi ya nardo kila mahali nyakati za siku zake za mwisho ulimwenguni.
***
Version for printing
Downloads
Contact us
Webmaster