GT Bible Studies    

    Swahili    


Navigation Glad Tidings Bible Studies in Swahili

11. MUUMINI ANAYEAMINI SHINGO UPANDE (Mk 9:14 - 29)



TAARIFA MUHIMU: Mtu aliye na pepo mbaya husemekana kuwa amepagawa. Hii ni hali tofauti na kuwa na ugonjwa wa akili au kifafa n.k. Pepo mbaya hawezi kumwingia mtu anayemwamini Yesu na aliyebatizwa kwa jina lake kwa sababu Roho Mtakatifu tayari anaishi moyoni mwake. Kulingana na Luka, kijana katika kifungu hiki alikuwa mtoto wa pekee wa wazazi wake (Lk 9:38).

1. Yafikirie maisha ya kila siku ya baba huyu yalivyokuwa tangu mwanawe alipopagawa na upepo mwovu (17 - 18, 20 - 22). (Ufikirie uhusiano kati yake na mkewe ulivyokuwa, yeye na watoto wake wengine, yeye na majirani na yeye na Mungu. Hofu yake ilikuwa nini kuhusu maisha ya baadaye ya familia yake? Ni majaribio gani aliyokuwa ameyafanya ili kumfanya mwanawe aponywe?)

  • Yalinganishe maisha ya kijana huyu na ya wenzi wake (17 - 18, 20 - 22).

    2. Shida kubwa sana kwa baba huyu ilikuwa ipi kulingana na hali inayoelezewa katika aya ya 14 - 18?

    3. Yesu alikuwa anawazungumzia akina nani alipokizungumzia kizazi kisichoamini alichokipata kuwa kigumu sana kukivumilia (19)?

  • Kwa nini ilikuwa vigumu kwa Yesu kuvumilia kutoamini kwa watu katika hali hii (19)?
  • Je, unafikiri Yesu angekiitaje kizazi hiki chetu?

    4. Kwa nini baba alijijumuisha katika kilio cha mwanawe ili kutaka msaada: "Tuhurumie na tusaidie!" (22)?

    5. Katika aya ya 23, Yesu anaonekana akiidai imani thabiti kutoka kwa baba. Kwa nini alifanya hivyo?

  • Ungehisije iwapo mtu angedai imani kamili kutoka kwako wakati ungekuwa na mfadhaiko ?

    6. Baba alikiamini nini na alikishuku nini alipokuwa akiipaaza sauti ya ombi lake katika aya ya 24?

  • Ulikiamini nini na ulikishuku nini ulipoulilia msaada wa Yesu mara ya mwisho kuhusu shida za wapendwa wako?

    7. Je, kilio hiki cha msaada kilithibitisha kuwa tayari baba alikuwa na imani ya wokovu au la (24)? Toe sababu zako.

  • Unafikiri baba alikuwa muumini wa Yesu lini? Ujadili uwezekano mbali mbali.

    8. Kwa nini Yesu aliisaidia familia hii ingawa baba wala mwanawe hakuwa na imani thabiti (25)?
  • Ni kwa imani ya nani muujiza huu ulifanyika?
  • Ni kiasi gani cha imani kingehitajika ndipo Yesu aweze kuwasaidia wapendwa walio katika mateso?

    9. Inaelekea kuwa baba alifikiria kuwa mwanawe tayari alikuwa amekufa alipolala chini kama maiti (26). Kwa nini aliupata uzoefu huu wa mateso sana kabla ya Yesu kumsaidia. (Baba angekosa kujifunza nini kama angesaidiwa na Yesu papo hapo?)
  • Kwa nini mara kwa mara Yesu anaturuhusu tufikie hali ya kuikata tamaa kabla ya yeye kuingilia kati?

    10. "Yesu alimshika mkono na akamsimamisha" (27). Liweke jina la mtu unayesumbuliwa naye katika sentensi hii. Aya ya 27 inakwambia nini unapoisoma jinsi ilivyo?

    11. HABARI NJEMA: Hata wakati watu waovu na pepo wabaya walimtesa Yesu, bado aliuamini uwezo na upendo wa Baba yake wa Mbinguni kwa imani thabiti. Kwa sababu ya imani yake kamili, sisi pia tunaweza kuupokea msaada wake licha ya mashaka yetu.

    ***

    Version for printing    
    Downloads    
    Contact us    
    Webmaster