GT Bible Studies    

    Swahili    


Navigation Glad Tidings Bible Studies in Swahili

8. WAKATI TENDO LISILOWEZEKANA LINATENDEKA (Mk 5:21 - 24 na 35 - 43)



TAARIFA MUHIMU: Kwa kawaida, mkuu wa sinagogi alichaguliwa kutoka miongoni mwa watu walioheshimika mjini. Watawala wa sinagogi wengine wote katika injili zote nne walikuwa wapinzani wa Yesu isipokuwa Yairo. Mtu huyu alikuwa na binti wa pekee tu (Lk 8:42).

1. Yafikirie maisha ya kila siku ya familia hii ndogo baada ya mtoto waliyemngojea kwa muda mrefu kuzaliwa. (Wazazi walihisije walipogundua kuwa mtoto alikuwa msichana na si mvulana? Ni ndoto gani walizokuwa nazo katika maisha ya baadaye ya binti yao?)

2. Ni nini kinachoweza kutokea kwa uhusiano baina ya wazazi na mtoto wao anapokuwa mgonjwa? Zifikirie sababu tafauti tofauti.

  • Yairo alifikiria nini kuhusu Mungu binti yake alipokuwa mgonjwa?

    3. Kwa nini Yairo aliamua kuutaka msaada kutoka kwa mtu ambaye marafiki zake wote walimchukia?

  • Yairo alihisi nini kuhusu Yesu wakati huu kutokana na alivyomhutubia (22 - 23)?

    4. Fikiria alivyohisi baba alipoipokea habari mbaya kutoka nyumbani (35).

  • Iwapo umewahi kuhisi kuwa unamsumbua Yesu, hayo yalitokea lini?

    5. Kwa nini Yesu alimwambia Yairo asiogope ingawa jambo baya sana lilikuwa limetokea kwake (36)?

  • Inawezekana kuwa Yairo aliamini nini hata baada ya bintiye kufa?

  • Yairo angekuwa amefanya nini kama hangekuwa amemwamini Yesu?

    6. Ni nini unachokiogopa sana ulimwenguni? (Unaweza kujibu kimoyomoyo.)
  • Ungefanya nini kama Yesu angekwambia usiogope wakati jambo baya zaidi limetendeka kwako?

  • Yesu anakuambia leo, "Usiogope, amini tu". Maneno haya yana maana gani katika hali yako ya sasa?

    7. Mkewe Yairo alimwona bintiye akifa wakati mumewe alipokuwa hayuko nyumbani. Hali yake ya kiakili ilikuwaje wakati Yesu na mumewe waliwasili nyumbani?

  • Mipango ya mazishi ilikuwa ikiendelea Yesu alipowasili katika nyumba ya Yairo (38). Yesu alitaka kuwaambia wageni nini kulingana na maneno yake yapatikanayo katika aya ya 39?

    8. Soma kwa makini jinsi Yesu alivyomfufua msichana kutoka kwa wafu (41 - 43). Ni maelezo ya kina yepi unayoyapata kuwa muhimu?

    9. Kwa nini Yesu aliyatoa maagizo makali kwa watu wasimwambie yeyote kuhusu muujiza huu ingawa lingekuwa tangazo zuri kwa mahubiri yake (43)?

    10. Tukio hili lilikuwa na athari gani kwa msichana huyu mwenyewe? Liliathiri vipi maisha yake ya baadaye?

  • Maisha ya wazazi yalibadilikaje baada ya tukio hili?
  • Unafikiri familia hii ilifikiria nini kuhusu uvumi wa kufa na kufufuka kwa Yesu waliousikia baada ya mambo hayo kutokea?

    11. HABARI NJEMA: "Usiogope, amini tu" Yesu anasema kwa kinywa chake: "Niachie haya. Ninaweza kuyashughulikia." Yesu mwenyewe alikiogopa kitu kimoja tu, yaani kutenganishwa na Baba yake wa Mbinguni. Aliogopa sana hadi akatokwa jasho la damu huko Gethisemane. Kwa njia hii alituonyesha kuwa kutenganishwa na Mungu (yaani: jahanamu) ndicho kitu cha pekee tupaswacho kukiogopa. Misiba mingine yote anaiweza na itaweza kubadilika ikawa baraka katika maisha ya wale wamwaminio.

    ***

    Version for printing    
    Downloads    
    Contact us    
    Webmaster