GT Bible Studies    

    Swahili    


Navigation Glad Tidings Bible Studies in Swahili

6. MAFUNDISHO ZAIDI YA YESU: MWANA MPOTEVU MWINGINE (Lk 15:25 - 32)



TAARIFA MUHIMU: Kusema kweli, baba alikuwa ameiacha nusu ya mali yake kwa mwanawe mkubwa wakati kijana mdogo aliupokea urithi wake (aya ya 12). Halikuwa kosa la baba kwa mwanawe kutoyaamini maneno yake.

1. Kijana anaweza kufurahi iwapo anahisi kuwa wazazi wake hawampendi?

  • Kwa nini kijana mkubwa hakutoka nyumbani aende katika nchi za mbali na nduguye, iwapo alikuwa hayafurahii maisha yake nyumbani?
  • Unafikiri kijana mkubwa alikitamani kitu gani kuliko kitu chochote katika maisha yake?

    2. Kwa nini mwana mkubwa alijiona mwenyewe kama mtumwa ingawa babake alikuwa amemwahidi nusu ya mali yake (12b, 29, 31)?
  • Iwapo baba katika mfano huu ni Mungu na kijana mdogo ni mtu aliyetengana na imani yake ya Kikristo, unafikiri kijana mkubwa anamwakilisha nani?

  • Je unafikiri baba huyu aliwatendea wanawe haki?

  • Je unafikiri daima Mungu hututendea sisi watu wake haki?

    3. Kijana mkubwa alikuwa akifikiria nini alipokuwa akifanya kazi shambani kila siku?
  • Iwapo umejihisi sawa na alivyojihisi mwana huyu katika aya ya 29 - 30, ni katika hali gani hayo yalitokea?

  • Ni sababu gani halisi ambayo ilimfanya kijana mkubwa kutowafanyia marafiki zake sherehe (29)?

  • Baba angechukuliaje iwapo kijana mkubwa angekuwa amemchinja mbuzi, kondoo au ndama na kusherehekea na marafiki zake (30 - 31)?

    4. Ni sababu gani kubwa iliyomfanya kijana mkubwa kuwa na hasira katika hali hii (27 - 28)?

  • Kijana mdogo alikuwa amemwaibisha babake mbele ya kijiji kizima na sasa kijana mkubwa anafanya vivyo hivyo? Kwa nini babake hakukasirika?

  • Unaipata picha gani kumhusu huyu baba katika aya za 28b na 31 - 32?

  • Unaipata picha gani kumhusu Mungu katika aya za 28b, 31 - 32?
    5. Kwa nini kijana mkubwa hakumpenda babake ingawa daima baba alikuwa mwema kwake?
  • Jadilianeni katika msingi wa mfano huu: Ni sababu gani inayoweza kutufanya tusimpende Mungu?

    6. Kijana mkubwa alifikiria kuwa daima aliyatimiza mapenzi ya babake (29). Baba alitarajia nini kutoka kwa mwanawe kuliko vyote?
  • Ni nini kituonyeshacho kuwa kijana mkubwa kamwe hakumpenda nduguye mdogo (30)?
  • Kijana mkubwa alimpenda nani?
    7. Kwa nini Yesu aliukatisha mfano wake bila kutuambia iwapo Kijana mkubwa alihudhuria sherehe au la (28, 32)?
    8. Katika mfano wa Yesu, daima karamu inamaanisha mbinguni. Kulingana na mfano huu, ni nani atakayeingia mbinguni mwishowe?

  • Litakuwa kosa la nani ikiwa mtu fulani hataingia mbinguni kulingana na mfano huu?

    9. Ifikirie hali ambapo vijana hawa wawili walikwenda shambani asubuhi iliyofuatia. Hali ya ndugu mkubwa ingekuwaje na ya ndugu mdogo je?

  • Watu wote duniani wanafanana na ndugu mkubwa au mdogo katika mfano huu. Unafikiri unafanana na yupi? (Unaweza kujibu kimoyomoyo.)

    10. MASWALI YA HABARI NJEMA: Yesu anakwambia: "Vyote vilivyo vyangu ni vyako." Msalabani, alikuweka mahali mbinguni. Alikupatia urithi huu siku ile ulibatizwa. Ndugu mkubwa hakuiamini ahadi hii lakini aliushughulikia urithi wake kama mtumwa. Je, unaamini kuwa utaupokea urithi wako wa mbinguni bure au unajaribu kuupokea kwa matendo yako mema? Unaweza kujibu kimoyomoyo.)

  • (Kwa kila mshiriki kujibu): Ni jambo gani muhimu sana ulilojifunza kutokana na haya Mafundisho ya Biblia?
    ***

    Version for printing    
    Downloads    
    Contact us    
    Webmaster