5. MAFUNDISHO YA YESU: MWANA MPOTEVU (Lk 15:11 - 24)
TAARIFA MUHIMU: Hadithi iliyotolewa na Yesu inaitwa mfano. Urithi haukupokewa wakati baba alikuwa angali hai. Nyakati za Yesu, nyumba haikusimama peke yake kilimani bali ilijengwa kijijini karibu na barabara nyembamba. Pahali pa pekee ambapo ungeweza kusimama ili uone nje ya kijiji palikuwa juu ya paa la nyumba (20). Jinsi tulivyokwisha kusema awali, wamaume hawakuwakimbilia wanaume wenzao katika sehemu hizo za ulimwengu.
1. Kijana anaweza kufurahi iwapo wazazi wake watauwekea uhuru wake mipaka?
Kwa nini mwana mdogo hakuwa na furaha ingawa alikuwa na makao mazuri na baba mwema?
Ungekuwa katika nafasi ya baba, ungemjibu mwanao nini kuhusu ombi lake (12a)?
2. Kwa nini baba aliyaficha masikitiko na mahangaiko yake ingawa alifahamu vizuri kile ambacho kingetokea iwapo angemruhusu mwanawe atoke (12b)?
Katika mfano huu, Baba ni Mungu. Kijana anaweza kuwa mtu ambaye amemwacha Mungu baada ya kumwamini au baada ya kubatizwa kwa jina lake. Kwa nini Mungu hamzuii mwanawe anayemwacha?
3. Kwa nini vijana wengi wa siku hizi wanavutiwa na maisha mtindo ya kijana huyu - wanapokuwa ng’ambo peke yao bila wajibu wala pesa nyingi za matumizi?
Kijana huyu alizitumiaje pesa za babake: tazame aya ya 13 na 30.
Kwa nini kijana huyu hakupata marafiki wa kweli ambao wangebaki naye hata baada ya kuishiwa?
4. Nguruwe alichukiliwa kuwa mnyama mchafu miongoni mwa Wayahudi. Kijana huyu alifikiria nini alipoitafuta kazi ya kuwalisha nguruwe (14 - 15)?
Kwa nini kijana huyu hakuruhusiwa hata kukila chakula cha nguruwe ili kujishibisha (16)?
5. Ni nini kilichomfanya kijana huyu "kujirudi" badala ya kujinyonga alipokuwa katika hali hiyo ya kuikata tamaa (17)?
Katika aya ya 18-19, utalipata ungamo alilolipanga kijana huyu kumwambia babake. Dhambi zake kwa babake zilikuwa zipi?
Ni dhambi zipi ambazo mwana huyu alikuwa amezifanya "dhidi ya mbinguni" (18)?
Ni dhambi zipi ambazo umezifanya: a) dhidi ya mbinguni na b) dhidi ya wazazi? (Unaweza kujibu kimoyomoyo.)
6. Kwa nini kijan huyu hakutarajia kumwuliza babake amkubali kama mwanawe (19)?
Kwa kawaida ni watu wa aina gani wanaofikiria kuwa hawastahili kuitwa wana wa Mungu (19)?
7. Baba aliweza kufikiria nini alipomwona mwanawe akiikokota miguu yake barabarani kurudi kijijini akiwa hana viatu na isitoshe alivalia matambara (20)?
Ni nini kilichomfanya baba amtambue mwanawe kutoka mbali (20)? (Tazama taarifa muhimu.)
Unafikiri baba alikuwa akifanya nini miaka hii yote mwanawe alipokuwa mbali naye (20)?
8. Kwa nini mwana huyu hakumwambia babake mambo yote aliyokuwa ameyapanga kumwambia (18b - 19 na 21)?
Maneno na tabia za baba zilimwambia nini mwana huyu (22 - 23)?
Baba alimsamehea mwanawe lini? Taja aya.
Ni lini mwana huyu alianza kuuamini upendo na msamaha wa babake? Taja aya.
Maneno ya baba yalimaanisha nini katika aya ya 24?
9. Upendo wa Mungu unatofautianaje na ule wa wanadamu?
Mfano huu unafundisha nini kuhusu ubadilikaji?
10. MASWALI YA HABARI NJEMA: "Mwanangu alikuwa amekufa, kumbe yu hai." Pia Yesu aliiacha nyumba ya Baba yake na akaja humu ulimwenguni si kwa kuyaasi mapenzi ya Baba yake bali kuyatimiza. Wakati wa kurudi nyumbani, mlango wa mbinguni ulifungwa usoni pake na ilimbidi alie: "Mungu wangu, Mungu wangu mbona umeniacha?"Kwa nini kijana alikaribishwa namna ambavyo Yesu angekaribishwa katika mfano huu? Na kwa nini Yesu alikataliwa namna ambavyo mwana huyu angekuwa amekataliwa?
(Kwa kila mshirika kujibu): Ni jambo gani muhimu sana ulilojifunza kutokana na mafundisho ya kifungu hiki wakati huu?
***
Version for printing
Downloads
Contact us
Webmaster