GT Bible Studies    

    Swahili    


Navigation Glad Tidings Bible Studies in Swahili

3. YESU ANAKUTANA NA KAHABA (Luka 7:36 - 50)



TAARIFA MUHIMU: Aya ya 44-46 zinaelezea jinsi mgeni mashuhuri alivyopokewa nyakati za Yesu. Watu walikula wakiwa wameketi sakafuni; hiyo ndiyo sababu miguu michafu ya jirani ingemfanya mtu aipoteze hamu yake ya chakula. Kumbuka kuwa katika desturi za Wayahudi, mwanamke hakuzionyesha nywele zake mbele za wageni. Maana ya Mfarisayo ni muumini wa dhati wa Mungu. Simoni si yule aliyekuwa mwanafunzi wa Yesu.

1. Kwa maoni yako, kahaba anaweza kuishi maisha ya furaha? Zitoe sababu zako.

  • Watu wote katika mji huo walimjua mwanamke huyu aliyeuuza mwili wake wenyewe. Ufikirie uwezekano mbali mbali uliomfanya msichana huyu kuwa kahaba.

    2. Ni maadili gani yaliyokuwa muhimu katika maisha ya Simoni Mfarisayo?

  • Kwa nini Simoni hakumwuliza mmoja wa watumishi wake aioshe miguu ya Yesu; isitoshe, alikuwa amemwalika Yesu kuwa mgeni wake (36, 44 - 46).

  • Ni sababu zipi zilizokuwa zimemfanya Simoni amwalike Yesu kwake kwa chakula? Ufikirie uwezekano mbali mbali (36).

    3. Mwanamke anayezungumziwa aliwezaje kupenyeza hadi katika nyumba ya Simoni na hadi katika chumba cha kulia chakula? Ufikirie uwezekano mbali mbali.

  • Marimari yenye marhamu yalikuwa ya bei ghali. Mwanamke huyu aliyapataje marimari haya au alikuwa ameyanunua kwa sababu gani? Zifikirie sababu mbali mbali.

    4. Kwa nini mwanamke huyu alitaka sana kukutana na Yesu hadi akathubutu kuingia katika nyumba ya Mfarisayo, akijua wazi wazi kuwa angeshindwa?

  • Nyakati hizo watu wa dini hawakuchangamana na watenda dhambi. Ni nini kilichomfanya mwanamke huyu awe na matumaini kuwa Yesu angekuwa tofauti?

    5. Kwa nini mwanamke huyu alitaka kumgusa Yesu (38)?

  • Ni nini kinachofanyika iwapo panya, nyoka au mtu tunayemchukia anatugusa?

  • Mwanamke huyu alikuwa na uamuzi gani kutokana na ukweli kwamba Yesu hakuuogopa mguso wake?

    6. Kisia lini mara ya mwisho ambapo mwanamke huyu alikuwa amelia.

  • Ni machozi ya kiasi gani yanayohitajika ili mtu aweze kuiosha miguu ya mtu mwingine?

  • Ni nini kilichomfanya mwanamke huyu alie sana hadi miguu ya Yesu ikaloa?

  • Kwa nini mwanamke huyu hakuikausha miguu ya Yesu kwa skafu au pindo la nguo yake badala ya nywele zake?
  • Mwanamke huyu hakulinena hata neno moja wakati wa chakula; je, tabia zake zilionyesha nini?

    7. Katika aya ya 41 - 42, Yesu anautoa mfano mfupi kuhusu mtu mmoja mkopeshaji alikuwa na wadeni wawili. Mkopeshaji ni Mungu lakini Yesu anamsema nani anapowazungumzia hawa wadaiwa waiwili?

  • Yesu anazifananisha dhambi na deni. Deni la dinari 500 linalingana na mshahara wa mtu wa kawaida kwa mwaka mmoja na nusu. Deni la dinari 50 linalingana na mshahara wa mwezi mmoja na nusu. Hizi zingekuwa kiasi gani cha pesa katika sarafu zetu?

  • Hebu tuchukulie kuwa kila dhambi uliyoifanya inalingana na deni, tuseme yuro 10 50/shilingi 1,000. Unamwia Mungu pesa kiasi gani kufikia sasa? (Unaweza kujibu kimoyomoyo.)

    8. Kwa nini Simoni alimdharau Yesu na mwanamke yule?

  • Kwa nini ni rahisi kuziona dhambi za wengine kuliko zetu?

    9. Lipi lililotokea kwanza: Mwanamke huyu aliamini kwanza kuwa dhambi zake zilikuwa zimesamehewa au alimpenda Yesu kwanza ndipo dhambi zake zikasamehewa? Zitoe sababu zako kutoka aya za 42 - 43, 47.

  • Nani aliyelipa deni ambalo mwanamke huyu alimwia Mungu?

  • Ni nini kilichotokea kwa deni ambalo Simoni alimwia Mungu?

  • Yesu aliyalipa madeni ya watu wote kwa sarafu gani?

    10. MASWALI YA HABARI NJEMA: Yesu anazijua dhambi zako zote lakini licha yake anakwambia: "Umesamehewa dhambi zako zote. Imani yako imekuokoa. Nenda kwa amani!" (Aya ya 48 na 50). Ni yeye tu aliye na haki ya kuyasema maneno haya kwa sababu alilipia- deni ya dhambi zako kwa damu yake. Unamjibu nini? (Unaweza kujibu kimoyomoyo.)

  • (Kwa kila mshirika kujibu): Ni jambo gani muhimu zaidi ulilojifunza kutokana na haya mafundisho?

    ***

    Version for printing    
    Downloads    
    Contact us    
    Webmaster